Psalms 37:1-4

Mwisho Wa Mwovu Na Urithi Wa Mwenye Haki

(Zaburi Ya Daudi)


1
Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bUsisumbuke kwa ajili ya watendao maovu,
wala usiwaonee wivu watendao mabaya,

2 ckwa maana kama majani watanyauka mara,
kama mimea ya kijani watakufa mara.


3 dMtumaini Bwana na utende yaliyo mema;
Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

4 eJifurahishe katika Bwana
naye atakupa haja za moyo wako.

Copyright information for SwhKC